IQNA

Maandamano ya Siku ya Kuonyesha Uaminifu kwa Mapinduzi ya Bahrain

15:42 - June 22, 2011
Habari ID: 2142808
Wananchi wa miji mbalimbali ya Bahrain wameandamana tena leo wakipinga hukumu zilizotolewa na vyombo vya mahakama vya nchi hiyo dhidi ya viongozi wa kambi ya upinzani.
Makundi ya wanamapinduzi wa Bahrain yamesisitiza kuwa maandamano hayo yanafanyika leo kote nchini kupinga hukumu zinazotolewa na hamakama za kimaonyesho za utawala wa Aal Khalifa dhidi ya viongozi wa kambi ya upinzani.
Askari usalama wa Bahrain wamejizatiti katika maeneo muhimu ya miji ya nchi hiyo kwa ajili ya kukabiliana na waandanaji.
Inatazamiwa kuwa mahakama ya Bahrain leo itatoa hukumu ya kifo dhidi ya viongozi kadhaa wa maandamano ya amani ya wananchi wanaopinga utawala wa Aal Khalifa. Kwa sababu hiyo vyama na makundi mbalimbali ya Bahrain yameamua kufanya maandamano kulaani hukumu za mahakama hiyo.
Hadi sasa mahakama ya Bahrain imetoa hukumu ya vifungo jela dhidi ya raia kadhaa kwa kosa eti la kuchochea maandamano ya wananchi dhidi ya utawala wa nchi hiyo. 813451
captcha