Amesema matamshi yaliyotolewa na Sheikh Ahmad Tayyib katika uwanja huo yamebatilisha njama za Wazayuni za kutaka kuzusha mfarakano kati ya Waislamu.
Sayyid Ali Fadhlullah amesema matamshi yaliyotolewa na Sheikh wa al Azhar kuhusu Mashia ni ya kishujaa na yanaonyesha jitihada zake za kuimarisha umoja wa umma wa Kiislamu.
Mwana wa kiume wa Allamah Fadhlullah amesema matamshi yaliyotoleawa na Sheikh wa al Azhar ni hatua muhimu ya kuimarisha umoja na mshikamano wa Kiislamu ambayo pia yatabatilisha njama za Wazayuni za kutaka kuzusha hitilafu na migawanyiko baina ya Waislamu.
Sayyid Ali Fadhlullah ameongeza kuwa hatua ya Sheikh Ahmad Tayyib imechukuliwa kwa ajili ya kuimarisha safu za Waislamu na katika kipindi ambacho madola ya kibebeberu yanafanya njama za kuzusha hitilafu katika umma wa Kiislamu.
Taarifa hiyo imesisitiza kuwa msimamo huo wa Sheikh wa al Azhar umezima mipango ya maadui ya kuzusha fitina kati ya Waislamu wa madhehebu za Shia na Suni hususan baada ya kusema waziwazi kwamba Wasuni wanaswali nyuma ya Waislamu wa madhehebu ya Shia na kwamba milango ya Chuo Kikuu cha Al Azhar iko wazi kwa ajili wanafunzi wa Kishia. 823325