IQNA

Wasomi Waislamu kutoka nchi 10 kutoa Mihadhara Imarati Mwezi wa Ramadhani

19:05 - July 25, 2011
Habari ID: 2159815
Umoja wa Falme za Kiarabu umewakaribisha wanazuoni 35 wa Kiislamu kutoka nchi 10 kutoa mawaidha nchini humo katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Maulamaa walioalikwa ni kutoka Saudi Arabia, Bahrain, Morocco, Yemen, Misri, Syria, Mauritania, Pakistan, Malaysia na India ambao watakuwa wageni wa Rais Sheikh Khalifa bin Zayed Al Nahyan hadi mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Lengo la mpango huo limetajwa kuwa ni kustawisha thamani za Kiislamu, ukuruba, mitazamo ya wastani, kubadilishana mawazo na fikra na vilevile mawasiliano ya Waislamu wa Imarati na wageni. Dr. Hamdan Musallam al Mazrui Mkuu wa Halmashauri ya Masuala ya Kiislamu na Awqaf anayesimamia mpango huo amesema hotuba za wanazuoni hao wa kigeni zitachapishwa baada ya mwezi wa Ramadhani. Ametoa wito kwa vijana wa Imarati kushiriki katika mihadhara ya Mwezi wa Ramadhani na kukutana na wanazuoni hao wa kigeni.
831119
captcha