Rais Ahmadinejad ameongeza kuwa, lengo la Shirika la Utangazaji la Redio na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) linapaswa kuwa ni kusambaratisha mfumo wa kibeberu. Rais Ahmadinejad amesisitiza kwamba, vipindi vya Shirika la Utangazaji la Redio na Televisheni la Iran (IRIB) vinapaswa kuandaliwa kwa namna ambayo vitasambaratisha mfumo wa kibeberu na uwepo wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
Rais wa Iran ameashiria matukio mbalimbali yanayojiri hivi sasa ulimwenguni na kusisitiza kwamba, mfumo wa kibepari umo katika hali ya kusambaratika na kwamba, hauna uwezo tena kujiokoa na hilo. Rais Ahmadinejad ameashiria taathira chanya ya Mapinduzi ya Kiislamu katika matukio ya ulimwengu na kubainisha kwamba, ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ulihuisha thamani za mwanaadamu na kuleta mwamko kwa wananchi wa kupinga ubeberu na kudai haki zao.
834348