IQNA

Washindi wa Mashindano ya Qur'ani Nigeria waenziwa

17:20 - August 01, 2011
Habari ID: 2163309
Washindi wa Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani ya 'Al Maher' nchini Nigeria wametunukiwa zawadi katika sherehe zilizofanyika Julai 30.
Kwa mujibu wa gazeti la Al Riyadh, mashindano hayo yameandaliwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani kwa ushirikiano na Taasisi ya Utamaduni ya Sultan Amir. Mashindano hayo yalikuwa na washiriki 55 wa kike na kiume waliohifadhi Qur'ani.
Kulikuwa na vitengo vya kuhifadhi Qur'ani nzima, nusu ya Qur'ani na robo ya Qur'ani.
Jopo la majaji wanne wa kimataifa lilisimamia mashindano hayo.
834392
captcha