IQNA

1:34 - August 03, 2011
Habari ID: 2164301

Katibu Mkuu wa OIC atoa salamu za Ramadhani kwa Waislamu

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC Prof. Ekmeleddin Ihsanoglu ametoa salamu za kheri na fanaka kwa Waislamu wote kwa mnasaba wa kuwadia mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Katika salamu zake Ihsanoglu amesema: ‘Natoa salamu zangu za kheri na fanaka kwa Waislamu wote duniani na namuomba Mwenyezi Mungu akubali Saumu, Sala na amali zao njema. Kuwadia mwezi huu mtukufu ni wakati muafaka wa kusisitiza juu ya thamani aali za Kiislamu na umuhimu wa umoja wa Waislamu. Ni jambo la kusikitisha kuwa mwezi wa Ramadhani umewadia wakati maeneo kadhaa ya Waislamu duniani yanakumbwa na vita, masaibu na maafa ya kibinaadamu’.
Katibu Mkuu wa OIC pia ametoa wito kwa Waislamu duniani kuwasaidia Wasomali wanaokumbwa na maafa ya njaa.
835712
captcha