IQNA

17:29 - August 16, 2011
Habari ID: 2172102
Sayyid Ammar al Hakim:

Kurushwa hewani filamu ya al Hassan na al Hussain ni jinai dhidi ya binadamu

Mkuu wa Baraza Kuu la Kiislamu la Iraq Sayyid Ammar al Hakim amekosoa hatua ya kurusha hewani filamu ya al Hassan na al Hussain inayohujumu matukufu ya Waislamu wa madhehebu ya Shia katika kanali kadhaa za televisheni za Kiarabu na kusisitiza kuwa kurushwa hewani filamu hiyo ni jinai kubwa dhidi ya binadamu, Uislamu na Maimamu watoharifu katika kizazi cha Mtume Mauhammad SAW.

Mkuu wa Baraza Kuu la Kiislamu la Iraq amesema ni kosa lisilosameheka kuchochea wananchi na kuzusha fitina baina yao kwa kuchukua hatua kama hiyo. Ameongeza kuwa inashangaza kuona filamu hiyo ikirushwa hewani katika kanali nane za televisheni za Kiarabu tofauti kabisa na ada ya televisheni hizo ya kutorusha hewani filamu kama hizo.
Sayyid Ammar al Hakim amewashukuru wabunge wa Iraq kwa kupiga marufuku filamu hiyo kuonyeshwa katika televisheni za nchi hiyo na akasema filamu hiyo inachochea hitilafu za kimadhehebu na kuwachukiza Waislamu wengi wa Iraq.
Filamu hiyo ya al Hassan na al Hussain iliyotengenezwa nchini Jordan inapotosha ukweli wa mambo kuhusu historia ya wajukuu wa Mtume Muhammad SAW, Imam Hassan na Hussein AS na kutetea watu waliodhulumu na kuwaua watukufu hao. 844707
captcha