Kwa mujibu wa tovuti ya emaratalyoum, Mufti wa Saudia, Baraza la Maualmaa Saudia na vilevile Ali Gomaa, Mufti wa Misri siku ya Alkhamisi walitoa taarifa tofauti wakipinga taarifa kuwa sayari ya Zohali ndiyo iliyoonekana Saudia badala ya hilali ya mwezi wa Shawwal.
Baraza la Wanafalaki wa Jeddah nchini Saudia Arabia lilitangaza kuwa sayari ya Zohali ilitangazwa kwa makosa kuwa ndio hilali ya mwezi wa Shawwal na kwa hivyo watu wa Saudia walisherehekea idi kwa kuiona sayari hiyo.
Duru katika Baraza la Wanafalaki Jeddah zinasema kuwa katika kipindi hiki cha mwaka sayari ya Zohali inaweza kuonekana katika baadhi ya maeneo ya Saudia kwa teleskopu. Aidha wanafalaki hao wanasema kwa mujibu ya mahesabu ya kifalaki, haingewezekana hilali ya Shawwal kuonekana Saudi Arabia siku ya Jumatatu na hivyo kuonekana Zohali ndiko kulikopelekea kujiri tatizo kuhusu mwezi mwandamo.
853216