IQNA

12:52 - September 05, 2011
Habari ID: 2181520

Sheikh wa al-Azhar akataa ombi la kuhani wa Kiyahudi la kusamehewa Mubarak

Sheikh wa al-Azhar amekataa ombi la kuhani mmoja wa Kiyahudi anayefungamana na utawala haramu wa Israel la kumtaka atoe fatuwa ya kidini ya kusamehewa dikteta wa zamani wa Misri Husni Mubarak.

Sheikh Ahmad Tayyib ametupilia mbali ombi hilo la Kuhani Aufadya Yusuf, Mkuu wa Baraza la Wanazuoni wa Torati akisema kuwa al-Azhar haitajibu matamshi na maombi ya makuhani wa Kizayuni kuhusiana na Mubarak wala kufanya nao mazungumzo kuhusiana na jambo hilo. Amesema kufanya mazungumzo na makuhani hao wenye misimamo mikali ya Kizayuni ni sawa na kulegeza msimamo wa al-Azhar kuhusiana na utawala haramu wa Israel, jambo ambalo chuo hicho cha kidini hakiko tayari kulifanya.
Ombi hilo la makuhani wa Kizayuni limewashangaza wengi katika ulimwengu wa Kiislamu kwa sababu halikutarajiwa kabisa katika mzingira tata ya hivi sasa nchini Misri. Kuhani aliyetajwa wa Kizayuni ameitaka pia serikali ya Marekani kutoa mashinikizo ya kisiasa dhidi ya viongozi wa kijeshi wa Misri ili waepushe kuhukumiwa kifo dhidi ya dikteta Mubarak.
Kuhani Yusuf pia amemtaka Rais Shimon Peres wa utawala haramu wa Israel aingilie kati na kuutaka Umoja wa Ulaya utoe mashinikizo dhidi ya serikali ya mpito ya Misri ili kuifanya imwachilie huru Mubarak.
Kuhani huyo ni rafiki mkubwa wa Mubarak ambaye kila mwaka amekuwa akimpongeza dikteta huyo wa Misri kwa mnasaba wa kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwake. 854280
captcha