IQNA

12:44 - September 08, 2011
Habari ID: 2183492

Sheikh Qardhawi: Kuanguka madikteta ni kwa mujibu wa suna ya Mwenyezi Mungu

Sheikh Yusuf Qardhawi Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Maulamaa Waislamu amesema mapinduzi yanayojiri katika baadhi ya nchi za Kiarabu ambayo yamepelekea madikteta kuanguka ni jambo la kawaida ambalo linaenda kwa mujibu wa suna na kanuni za Mwenyezi Mungu.

Kwa mujibu wa gazeti la Al Khabar la Algeria, Sheikh Qardhawi amesema: “Lakabu ya ‘Mwamko wa Kiislamu’ yaliyopewa matukio ya mapinduzi hayo inatosha na ni nani aliyefikiri matukio haya yatajiri”.
Akizungumza mbele ya hadhara ya vijana, Sheikh Qaradhawi mwenye makao yake huko Doha, Qatar ameongeza kuwa: “Baada ya utawala wa Maliberali na Wasekula, sasa umefika wakati wa wanaharakati wa Kiislamu. Ni muhimu wanaharakati wa Kiislamu watafakari namna ya kuchukua kwa mara nyingine uongozi wa dunia”.
Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Maulamaa Waislamu amesema Misri sasa iko tayari kuanzisha serikali ya Kimataifa ya Kiislamu.
Amesema kinyume na mifumo ya Kiliberali na Kisekula, mfumo wa Kiislamu hautakuwa na hadaa wala ufisadi bali ni wakati wa sayansi, amali njema na bidii.
856762
captcha