IQNA

15:01 - September 11, 2011
Habari ID: 2184952

Tukio la Septemba 11, juhudi za kuudhibiti ulimwengu wa Kiislamu

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya mji mtakatifu wa Najaf nchini Iraq, amesisitiza kwamba tukio la Septemba 11 lilitekelezwa kwa makini kwa shabaha ya kuudhibiti ulimwengu wa Kiislamu kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi.

Hayo yamesemwa na Hujjatul Islam wal Muslimeen Sayyid Swadr Deen Qubanchi, khatibu wa Swala ya Ijumaa ya mjini Najaf alipokuwa akizungumza katika Husseiniya ya Fatimat al-Kubra. Amesema tukio la Septemba 11 lililopelekea kuvamiwa nchi mbili za Kiislamu za Afghanistan na Iraq lilifanyika kwa mpangilio maalumu wa nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani kwa ajili ya kuudhibiti Ulimwengu wa Kiislamu na Waislamu.
Amesema licha ya njama zilizofanywa na mabeberu hao wa Magharibi kwa ajili ya kuwadhibiti Waislamu, lakini hali ya mambo hasa katika Mashariki ya Kati imebadilika kwa maslahi ya ulimwengu wa Kiislamu ambapo madikteta ambao wamekuwa wakiwakandamiza Waislamu wameng'olewa madarakani.
Sayyid Qubanchi ametaka kutekelezwa mara moja kwa mpango wa amani kati ya Marekani na Iraq ambapo askari wa nchi hiyo ya Magharibi wanatakiwa kuondoka nchini Iraq ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, na kuvunjilia mbali madai ya wale wanaodai kwamba Iraq inaweza kutumbukia kwenye dimbwi la machafuko ya ndani baada ya kuondoka askari vamizi wa Marekani nchini humo. 857802
captcha