Katika kikao hicho, wanafikra na maulamaa hao wa madhehebu mbalimbali ya Kiislamu waliamua kwamba watakuwa wakikutana mara kwa mara kwa ajili ya kuchunguza na kutatua matatizo na vikwazo vinavyozuia kupatikana umoja na mshikamano miongoni mwa madhehebu ya Kiislamu.
Akizungumzia suala hilo Mahmoud Ashur, Mkuu wa Taasisi ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu ya Kiislamu ya Misri amesema kuwa licha ya kwamba kuna tofauti za kifik'hi kati ya madhehebu tofauti ya Kiislamu lakini jambo hilo halipasi kuchukuliwa kuwa kikwazo kinachuzuia kufikiwa umoja na ushirikiano kati ya Waislamu kuhusiana na masuala wanayoafikiana.
Ahmad al-Ghamrawi, Mkuu wa Jumuiya ya Urafiki wa Misri na Iran naye amesema kwamba miongoni mwa njama zinazotekelezwa dhidi ya Waislamu ni pamoja na kudhoofisha na kuharibu kabisa nchi za Kiislamu, kuvuruga uhusiano wao na vilevile kudhoofisha uhusiano wa kijamii wa Waislamu. 861883