Kwa mujibu wa gazeti la Irish Times, mbunge huyo amesema kuwa Uholanzi inapasa kufuata mfano wa Uswisi kwa kuandaa kura ya maoni na kisha kupiga marufuku ujenzi wa minara ya misikiti nchini humo.
Wilders ambaye alikuwa akizungumza bungeni siku ya Alkhamisi tarehe 22 Septemba kwa mara nyingine tena amekariri matamshi yake ya dharau na kukosea heshima matukufu ya Kiislamu kwa kudai kuwa minara ni nembo zinazoeneza fikra za msituni, ukoloni na ubeberu.
Wilders ambaye mwaka 2008 alitengeneza filamu ya kutusi matukufu ya Kiislamu aliyoipa jina la Fitna na hivyo kuamsha hasira ya Waislamu kote duniani, anafahamika vyema kwa vitendo na msimamo wake ulio dhidi ya Uislamu na Waislamu.
Mwaka 2009 wananchi wa Uswisi walipiga kura ya maoni na kupiga marufuku ujenzi wa minara ya misikiti nchini humo. 866251