IQNA

19:30 - September 28, 2011
Habari ID: 2195241

Umoja wa Ulaya wataka kukomeshwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi Quds Mashariki

Mkuu wa siasa za nje wa Umoja wa Ulaya ameutaka utawala wa Kizayuni wa Israel kufuta kibali cha ujenzi wa nyumba mpya 1100 katika eneo la Baitul Muqaddas Mashariki.

Catherine Ashton ameliambia Bunge la Ulaya kwamba Israel inapaswa kufuta kibali cha ujenzi wa nyumba 1100 za walowezi wa Kiyahudi katika eneo linalokaliwa kwa mabavu la Baitul Muqaddas Mashariki.
Ashton ameelezea kusikitishwa kwake na kuendelea ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina na kusisitiza kuwa ujenzi huo unakwamisha mazungumzo ya amani.
Kwa upande wake Marekani imeutaja mpango huo wa Israel wa kuidhinisha ujenzi wa nyumba mpya za walowezi wa Kiyahudi katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Israel kuwa inakatisha moyo. 869125
captcha