IQNA

Kuvunjiwa heshima wanawake wa Bahrain, ishara ya kupotoka kimaadili utawala wa Aal Khalifa

16:51 - October 01, 2011
Habari ID: 2196699
Ayatullah Sheikh Isa Qassim, kiongozi wa Mashia wa Bahrain alisema jana Ijumaa kwamba vitendo vya dharau na kukosewa heshima wanawake wanamapinduzi, vinavyofanywa na utawala wa nchi hiyo vimesababisha machungu ambayo kamwe hayatasahauliwa na taifa la nchi hiyo.
Amesema vitendo hivyo vinavyoshabihiana na vya zama za ujahili vinaashiria wazi kupotoka kimaadili watawala wa ukoo wa Aal Khalifa.
Akizungumza jana katika swala ya Ijumaa huko katika Msikiti wa Imam Swadiq (as) katika eneo la a-Diraz, Ayatullah Qassim Isa amesema jinai na ugaidi unaotekelezwa na ukoo huo wa kifalme hautaogopesha wananchi na kuwafanya wasifuatilie matakwa na haki zao za kimsingi, bali utawatia zaidi moyo wa kufuatilia haki hizo.
Ayatullah Isa ameendelea kusema kuwa marekebisho halisi si matarajio tu kwa Wabahrain bali ni dharura ambayo hawawezi kuipuuza. Amesema wananchi hao wameamua kufanya mapinduzi ili kuishi kwa uhuru katika nchi yao na kujiamulia mustakbali wao wa kisiasa. Amesema jambo hilo litathibiti tu kwa kubuniwa katiba mpya iliyosimama juu ya msingi wa mantiki.
Ayatullah Qassim amewataka askari wa Bahrain na Saudia Arabia kukoma kuwavunjia heshima wanawake wanamapinduzi wa Bahrain na kuongeza kuwa utawala wa Aal Khalifa umekuwa ukidumisha kwa miaka mingi vitendo vya mabavu dhidi ya Wabahrain lakini kwamba jambo hilo halijawavunja moyo bali limeimarisha zaidi azma yao ya kuendelea kupigania haki zao. 870407
captcha