Akibainisha suala hilo, al-Husseini amesema kwamba viongozi hao dhalimu na vibaraka wanafanya njama dhidi ya mapambano ya Kiislamu na kupuuza ushindi wake badala ya kuyaunga mkono. Amesema katika hali ambayo utawala haramu wa Israel wenyewe unakiri kushindwa na harakati za mapambano hayo ya Kiislamu, watawala vibaraka wa Kiarabu wanapuuza ushindi wa mapambano hayo na kusimama dhidi ya wanamapambano.
Mbunge huyo wa Yemen amesema ni watawala haohao ndio hawakuwa na tatizo lolote na taghuti Shah wa Iran kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu lakini waligeuka na kuchukua msimamo wa kiuadui dhidi ya mapinduzi hayo yaliyoongozwa na hayati Imam Khomeini (MA). Walianza kufanya njama chungu nzima dhidi ya Iran ambayo ilianza kupeperusha mjini Tehran bendera ya ukombozi wa Palestina badala ya ile ya utawala haramu wa Israel iliyokuwa ikipeperushwa na Shah.
al-Husseini ameashiria uungaji mkono mkubwa wa watu wa Yemen kwa mapambano ya Palestina na kusema kuwa wananchi hao walishiriki kwa wingi katika maandamano ya kimataifa ya Siku ya Quds licha ya kukabiliwa na machafuko ya ndani. 871930