IQNA

16:22 - October 08, 2011
Habari ID: 2199882

Imam wa Awamiya awaomba vijana wa mji huo wawe watulivu

Nimri an-Nimr, Imam wa jamaa katika mji wa Awamiya mashariki mwa Saudi Arabia amewataka vijana wa mji huo wanaokandamizwa na utawala wa Saudia Arabia kuwa watulivu katika mazingira magumu yanayowakabili.

Akizungumzia matukio ya hivi karibuni ambapo askari usalama wa nchi hiyo walivamia eneo hilo lenye wakazi wengi wa Kishia na kuwatia nguvuni wanaharakati kadhaa wa kutetea haki za binadamu, Imam an-Nimr amewataka vijana wa eneo hilo kuwa watulivu na kukabiliana kwa uangalifu mkubwa zaidi, na matukio ya hivi karibuni yaliyopelekea vijana 14 kujeruhiwa.
Amewataka vijana hao kujiepusha kutumia nguvu katika kupigania haki zao kwa sababu jambo hilo amesema linakwenda kinyume na mafundisho ya Ushia. Amesema kwamba risasi haipaswi kujibiwa kwa risasi kwa sababu maneno na matamshi ni makali zaidi kuliko silaha.
Wakati huohuo Imam Nimri an-Nimri amewalaumu vikali askari usalama wa Saudia kwa kuchochea na kuwakandamiza vijana wa Kishia kwa kuwafyatulia risasi bila sababu yoyote ya maana, lakini pamoja na hayo amewataka vijana hao kuwa watulivu mbele ya uchokozi huo.
Kufuatia maandamano makubwa yaliyofanyika katika mji mwingine wa Qatif kwa ajili ya kuunga mkono maandamano ya Awamiya, askari usalama wa Saudia wamewafyatulia risasi moja kwa moja waandamanaji na kujeruhi vibaya 10 kati yao pamoja na kuwatia nguvuni wengine wengi. 874097
captcha