IQNA

15:26 - October 12, 2011
Habari ID: 2203859

Baraza la Usalama la UN lachunguza muswada dhidi ya Rais wa Yemen

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo linachunguza rasimu ya muswada dhidi ya dikteta wa Yemen Abdullah Saleh ambayo imetayarishwa na Uingereza.

Rasimu hiyo inachunguzwa baada ya mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen Jamal Umar kuwasilisha ripoti kuhusu hali ya nchi hiyo katika kikao kilichofanyika kwa faragha.
Baada ya ripoti hiyo Uingereza na nchi nyingine kadhaa zilitayarisha rasimu hiyo na kuiwasilisha katika Baraza la Usalama.
Wakati huo huo mwakilishi wa Ujerumani katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa wakati umewadia kwa Baraza la Usalama kuchukua hatua dhidi ya utawala wa Yemen. Amesema Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linapaswa kuchukua hatua kali na kumtaka Rais Abdullah Saleh wa Yemen atie saini mpango wa suluhu uliotayarishwa na Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi.
Ali Abdullah Saleh ambaye anaiongoza Yemen kwa kipindi cha miaka 33 amekataa mpango huo wa nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi. 878368

captcha