Kongamano hilo litafanyika kwa lengo la kupambana na ubaguzi unaofanywa dhidi ya Waislamu na kuwazindua wananchi kuhusu hatari ya jambo hilo katika jamii.
Msemaji wa Kituo cha Kiislamu cha Uswisi Qasim Elly, Mswisi aliyeingia katika dini ya Kiislamu miaka kadhaa iliyopita, amesema kongamano hilo ni hatua muhimu katika njia ya kupambana na ubaguzi unaofanywa dhidi ya Waislamu na hujuma ya kuwatisha watu kuhusu dini ya Kiislamu. Amesema kwamba inatazamiwa kuwa kongamano hilo litakuwa kubwa zaidi la Waislamu kuwahi kufanyika nchini humo.
Elly amesema kuwa kongamano hilo litakuwa fursa ya thamani kwa ajili ya shughuli za Baraza la Kituo cha Kiislamu cha Uswisi na kwa ajili ya kuonyesha jinsi linavyofanya bidii katika kutetea haki za kimsingi za Waislamu katika jamii ya Uswisi.
Amesisitiza kuwa kongamano hilo linaungwa mkono na kupata himaya ya watu na taasisi mbalimbali akiwemo dada wa mke wa Tony Blair, waziri mkuu wa zamani wa Uingereza aliyesilimu mwaka mmoja uliopita na mwandishi habari Muingereza Ivan Redly.
Kongamano hilo litahudhuriwa pia na viongozi na shakhsia muhimu wa Kiislamu kutoka nchi mbalimbali za Ulaya. 885397