IQNA

'Muslim News', mwakilishi wa magazeti ya Uingereza maonyesho ya kimataifa ya Tehran

11:34 - October 30, 2011
Habari ID: 2214203
Gazeti la Muslim News la Uingereza linashiriki katika Maonyesho ya Kimataifa ya Magazeti la Mashirika ya Habari kama mwakilishi wa magezeti ya Uingereza.
Msimamizi wa chumba cha gazeti la Muslim News katika maonyesho ya Tehran Zahra Kinji ameiambia IQNA kwamba amefurahishwa na kushiriki kwake katika maonyesho hayo na kwamba tukio hilo ni fursa nzuri kwa ajili ya kuanzisha ushirikiano kati ya magazeti na vyombo vya habari kutoka maeneo mbalimbali duniani.
Amesema gazeti la Muslim News linashughulikia habari za matukio mbalimbali na mitazamo ya Waislamu wa Britani.
Kuhusu mwangwi wa matukio ya sasa ya Mashariki ya Kati, mwamko wa Kiislamu na harakati ya kuteka Wall Street huko Marekani, Kanji amesema kuwa gazeti la Muslim News limeakisi habari za matukio hayo katika pande na mitazamo mbalimbali.
'Kuvunjiwa Heshima Qur'ani Tukufu katika Miji ya Marekani', 'Vita vya Iraq ni Kinyume cha Sheria', 'Hija na Umra', 'Kuenea Uislamu Britani' na 'Ubaguzi dhidi ya Wanawake Makazini' ni vichwa vya habari vya baadhi ya magazeti yanayoonyeshwa katika chumba cha gazeti la Muslim News la Uingereza katika Maonyesho ya Kimataifa ya Magazeti na Mashirika ya Habari mjini Tehran. 889432
captcha