IQNA

10:30 - October 31, 2011
Habari ID: 2214867

Maandamano ya 'Siku ya Ghadhabu na Watu Huru' kufanyika leo Bahrain

Wananchi wa Bahrain leo wanashiriki katika maandamano yaliyopewa jina la 'Siku ya Ghadhabu ya Watu Huru' kwa shabaha ya kusisitiza suala la kuachiwa huru wanamapinduzi wanaoshikiliwa katika korokoro za utawala wa Aal Khalifa.

Muungano wa Februari 14 wa Bahrain umetoa taarifa ukiwataka wananchi kushiriki kwa wingi katika maandamano ya leo na kuishinikiza serikali ya Manama ili iwaachie huru wapinzani na shakhsia wanaoshikiliwa katika jela za utawala wa nchi hiyo.
Wakati huo huo ripoti zinasema kuwa raia wengine kadhaa wa eneo la Bani Jamrah nchini Bahrain wametiwa nguvuni na askari wa utawala wa kifalme wa nchi hiyo ambao pia wamechoma moto nyumba na magari kadhaa ya wananchi. 890388
captcha