IQNA

15:52 - October 31, 2011
Habari ID: 2215202

Zawadi ya kumteka nyara askari wa Kizayuni yafikia dola milioni moja

Khalid bin Talal, mwanamfalme wa Saudi Arabia ameongeza zawadi ya dola laki moja iliyokuwa imetengwa na Sheikh Awadh al-Qarni kwa ajili ya kutekwa nyara askari mmoja wa Kizayuni, kwa dola nyingine laki 9 na hivyo kuifanya zawadi hiyo kuwa ya dola milioni moja za Marekani.

Khalid bin Talal ambaye ni ndugu yake Walid bin Talal, mwanamfalme mashuhuri na tajiri wa Saudia amesema kupitia mahojiano ya televisheni kwamba ameongeza kiasi cha fedha zilizotengwa na al-Qarni na kufikia dola milioni moja kwa ajili ya kutekwa nyara askari wa utawala haramu wa Israel.
Katika hali ambayo al-Qarani alitoa zawadi hiyo kwa ajili ya kutoa mashinikizo dhidi ya utawala wa Israel ili uwaachilie huru mateka wa Kipalestina, utawala huo umekasirishwa mno na kitendo hicho na kutangaza zawadi ya dola milioni moja kwa ajili ya kuuawa al-Qarni.
Inasemekana kuwa Khalid bin Talal ametangaza kuongeza zawadi hiyo kufikia dola milioni moja baada ya kukasirishwa na tangazo hilo na utawala wa Tel Aviv dhidi ya Sheikh al-Qarni.
Kwa upande wake, al-Qarni alitangaza zawadi ya kutekwa nyara askari wa Kizayuni baada ya walowezi wa Kizayuni kutangaza zawadi kubwa kwa mtu yoyote ambaye angemuua mmoja wa mateka wa Kipalestina walioachiliwa huru hivi karibuni na utawala wa Israel.
Sheikh Awadh al-Qarni ni mmoja wa mamufti wenye misimamo ya wastani wa Saudia ambao wanapinga vikali utawala wa Israel na kuunga mkono taifa la Palestina dhidi ya ukandamizaji wa utawala huo. 890431
captcha