IQNA

Upinzani wa Marekani wa kujiunga Palestina na UNESCO ni uadui dhidi ya utamaduni wa mataifa

17:25 - November 02, 2011
Habari ID: 2216527
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah, imetoa taarifa ikiipongeza Palestina kwa kupata uanachama katika Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) na kuongeza kuwa upinzani wa hivi karibuni wa utawala wa Marekani dhidi ya uanachama huo ni dalili ya wazi ya uadui wa nchi hiyo dhidi ya tamaduni za mataifa mengine.
Hizbullah imesema inataraji uanachama huo utakuwa mwanzo wa jamii ya kimataifa kutambua sehemu ya haki zilizoporwa za taifa la Palestina. Hizbullah imesema katika taarifa hiyo kuwa juhudi za Marekani, Canada na nchi nyinginezo za kupinga uamuzi wa kimataifa wa kuipa Palestina uanachama katika UNESCO ni uadui wa moja kwa moja wa nchi hizo dhidi ya mataifa ya Kiislamu na Kiarabu.
Imesema uadui huo ni juhudi za moja kwa moja za nchi hizo za kutaka kuyanyima mataifa mbalimbali haki zao za kimsingi.
Taarifa ya Hizbullah imesema hiyo ni dalili ya wazi inayoonyesha kwamba Marekani daima imekuwa ikitekeleza siasa za kibeberu na kimabavu na kutaka kuzitwisha fikra na mitzamo yake taasisi muhimu za kimataifa kwa madhara ya mataifa mengine ya duniani.
Huku ikilaani msimamo wa upinzani wa Marekani na waitifaki wake katika kupinga uanachama wa Palestina katika shirika la UNESCO, Hizbullah imesema kuwa jambo hilo linabainisha wazi kwamba uadui wa Marekani dhidi ya mataifa mengine sasa umevuka mipaka ya kisiasa na kuingia kwenye masuala ya kiutamaduni.
Imoeongeza kuwa jambo hilo si la kushangaza kwa kutilia maanani historian na rekodi mbaya ya ubaguzi ya nchi hiyo inayojaribu kupuuza na kufuta jamii nyinginezo. 891887
captcha