Msimamo huo umebainishwa katika kikao cha pamoja kilichofanyika jana mjini Cairo.
Maulamaa wa Kiislamu na Kikristo wa Misri wametangaza upinzani dhidi ya uingiliaji wa nchi za kigeni katika masuala ya ndani ya nchi yao kwa kisingizio cha aina yoyote katika kikao hicho kilichofanyika kwa hima ya Baraza la Taifa la Vijana.
Maulamaa hao wamesema kuwa taifa la Misri ni kiungo kimoja ambacho hakiwezi kutenganishwa na kwamba Wamisri wenyewe wanaweza kulinda umoja wao wa kitaifa. Wamesisitiza kuwa taifa la Misri linaelewa kuwa kuna mikono ya kigeni inayofanya njama za kuvuruga usalama wa taifa na kuharibu umoja nchini humo.
Washiriki katika mkutano huo wa Cairo wametoa taarifa ya pamoja wakisisitiza juu ya udharura wa kulindwa umoja kati ya raia wote wa Misri, Waislamu kwa Wakristo, na kusema kuwa wafuasi wa dini hizo mbili ni mwili mmoja katika kulinda nchi yao. 899433