Ayatullah Muhammad Emami Kashani ameongeza kuwa kama Waislamu wangekuwa wanazungumza kwa sauti moja hakuna dola lolote lingeweza kuwababaisha. Hata hivyo Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa hapa mjini Tehran amekumbusha kuwa bado kuna nafasi na uwezekano wa Waislamu kuungana na kuwa kitu kimoja.
Akizungumzia njama zilizofeli za Wamagharibi dhidi ya Iran, Ayatullah Kashani amesema maendeleo iliyopata Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kipindi chote cha vikwazo vya upande mmoja ndiyo yanayowatia kiwewe Wamagharibi.
Ayatullah Kashani pia amesema ripoti ya hivi majuzi ya IAEA dhidi ya Iran haina lengo lingine ghairi ya kuishinikiza zaidi Tehran lakini amesema taifa adhimu la Iran haliwezi kuyapigia magoti madola ya kishetani na yasiyomtegemea Mwenyezi Mungu.
900147