Akizungumza kabla ya kuanza mkutano huo wa siku tatu, David McLean mkurugenzi wa Mkutano wa Benki za Kiislamu amesema, 'katika miaka ya hivi karibuni mfumo wa kifedha wa Kiislamu umeimarika na kustawi kwa kasi katika kutoa huduma bora kimataifa'.
Amesema kongamano la mwaka huu litajadili 'Mashindano kwa ajili ya Ustawi wa Dunia' lengo likiwa ni kuimarisha kiwango cha mfumo wa Kiislamu wa fedha kote duniani. Amesema mkutano wa mwaka huu unahudhuriwa na wawakilishi kutoka nchi 50 duniani.
902264