Mabadiliko hayo ya bendera ambayo yalifanyika hapo jana Jumamosi yana maana kwamba bendera hiyo imechukua nafasi ya benderea nyekundu ambayo kwa kawaida hupepea kwenye kuba hiyo. Bendera hiyo nyeusi itapepea juu ya haram hiyo hadi Arubaini ya kuuawa shahidi Imam Hussein (as) na wafuasi wake wachache ambao waliuawa kinyama na maadui wa Uislamu katika jangwa la Karbala.
Baada ya kumalizika siku hizo arubaini, bendera hiyo nyeusi itaondolewa na ile nyekundu ya kawaida kurejeshwa. Bendera nyekundu ambayo hupeperushwa kwenye kuba ya Haram ya Imam Hussein huwa ni alama ya shahada na kujitolea mhanga kwa ajili ya kulinda dini tukufu ya Kiislamu.
Kila mwaka bendera ya Haram ya Abul Fadhlil Abbas (as) pia hubadilishwa sambamba na kubadilishwa bendera ya Haram ya Imam Hussein (as). 905787