Imesisitiza kwamba vikwazo hivyo ni hatari kubwa kwa taifa na serikali ya Syria. Taarifa ya Hizbullah imesema kwamba hatua hiyo iliyochukuliwa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu inakwenda kinyume na maazimio yake yenyewe yanayosisitiza umuhimu wa kuimarishwa ushirikiano kati ya nchi za Kiarabu. Imesema vikwazo dhidi ya nchi ndugu ya Syria ni aibu kubwa kwa ulimwengu wa Kiarabu na kutahadharisha dhidi ya kufanywa jumuiya hiyo kuwa chombo cha kudhamini maslahi ya Marekani katika nchi za Kiarabu.
Hizbullah imezihutubu nchi wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na kuzifahamisha kwamba vikwazo dhidi ya Syria ni dhulma kubwa kwa taifa na serikali ya nchi hiyo na kwamba havina faida nyingine yoyote ghairi ya kulinda na kutetea maslahi ya Wamagharibi na hasa Marekani katika Mashariki ya Kati. 907630