Kwa mujibu wa tovuti ya Al Intiqad, kikao hicho kimehudhuriwa na Maulamaa wa Kishia na Kisunni nchini Lebanon.
Kati ya waliohutubu katika hafla hiyo ni Sheikh Ibrahim Amin Al Seyyed Mkuu wa Idara ya Kisiasa ya Hizbullah na Sheikh Maher Hamud, Imamu wa Msikiti wa Quds katika eneo la Saida Lebanon na Sheikh Mohammad Amru mwanachama wa jumuiya hiyo.
Hafla hiyo imeandaliwa kwa mnasaba wa siku hizi za maombolezo ya kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume SAW, Imam Hussein AS akiwa na wafuasi wake 72 katika huko Karbala. Kongamano ambalo ni dhihirisho la umoja wa Kiislamu limefanyika katika Ukumbi wa Jumuiya ya Maulamaa Waislamu mjini Beirut.
908328