IQNA

16:02 - December 17, 2011
Habari ID: 2239133

'Madola ya kibeberu hayana budi ila kutambua haki za Iran'

Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema madola ya kibeberu hayana budi ila kutambua haki, heshima na adhama ya Wairani.

Akihutubia halaiki kubwa ya wananchi katika mji wa Yasouj kaskazini magharibi mwa Iran, Ahmadinejad amesema ni kwa maslahi ya nchi za kibeberu kufanya mazungumzo na taifa la Iran badala ya kuliwekea mashinikizo.
Rais Ahmadinejad amezikosoa baadhi ya nchi za Magharibi ambazo zina sera potofu kuhusu Iran. Amesema katika historia, Iran ndilo taifa huru zaidi ambalo daima limekuwa likipigania amani na uadilifu.
Amesema waliobuni ugaidi na mauaji duniani ndio leo wanaotoa madai yasiyo na ukweli wowote dhidi ya Iran. Rais wa Iran amewaonya mababeberu kuwa hawana nafasi katika mustakabali kutokana na sera zao potofu.
915457
captcha