Hafla hii imeandaliwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Umma Mmoja kwa lengo la kuenzi muqawama au mapambano ya taifa la Palestina. Baadhi ya Wapalestina walioachiliwa huru kutoka magereza ya utawala wa Kizayuni watahutubia kikao hicho kitakachofanyika Disemba 20.
Katika kikao hicho wanadiplomasia wanne wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wanaoshikiliwa mateka na utawala wa Kizayuni pia wataenziwa.
Itakumbukwa kuwa Oktoba 18 mwaka huu Utawala wa Kizayuni wa Israel umelazimika kukubali kuwaachilia huru mateka 1,027 wa Kipalestina kutoka katika jela zake mkabala wa kuachiliwa huru Gilad Shalit, mwanajeshi wa Kizayuni aliyekuwa akishikiliwa mateka na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS.
Wajuzi wa mambo wanaamini kuwa, kuachiliwa huru mateka wa Kipalestina kutahuisha tena muqawama wa wananchi wa Palestina na utawafanya Wapalestina kuwa na matumaini ya kuachiliwa huru mateka na wafungwa wengine elfu sita wa Kipalestina ambao wanashikiliwa katika magereza ya Wazayuni maghasibu.
Duru za kisiasa zinasisitiza kuwa, kutekelezwa mpango wa ubadilishanaji mateka baina ya Israel na Wapalestina kutazidi kuifanya HAMAS ipendwe na kusimama kwake kidete kusikochoka kuzidi kuthaminiwa.
917252