Kwa mujibu wa gazeti la Yaum as-Sabi' wanazuoni, wanachuo na vijana wanamapinduzi wa Misri walishiriki kwa wingi kwenye maandamano hayo na kutoa nara za kutaka wahusika wa mauaji hayo wafikishwe mahakamani na kisasi kutolewa dhidi yao kutokana na hatua yao ya kumuua Sheikh Imad Iffat, Katibu wa Dar al-Ifta pamoja na watu wengine waliouawa mbele ya ofisi ya Waziri Mkuu wa Misri.
Sheikh Ali Jumua, Mufti wa Misri pia alishiriki katika maandamano na mazishi hayo ya Sheikh Imad Iffat. Sheikh huyo aliuawa kwa njia ya kutatanisha alipokuwa akishiriki katika mkusanyiko wa Wamisri waliokusanyika mbele ya ofisi ya Waziri Mkuu kulalamikia siasa za wanajeshi wanaoongoza nchi hiyo.
Wamisri wamekuwa wakifanya mgomo mbele ya ofisi hiyo kwa muda wa wiki mbili sasa wakitaka Baraza la Wanajeshi livunjwe na wanapinga serikali mpya ya nchi hiyo inayoongozwa na Waziri Mkuu Kamal al-Janzuri. 917857