Mashindano hayo yameanza kwa qiraa ya Qur'ani Tukufu ya Mehdi Negahdar ambaye alichukua nafasi ya kwanza katika mashindano ya mwaka jana.
Akihutubu katika kikao hicho, Hujjatul Islam Moslem Yaqubi Mkurugenzi wa Kituo cha Darul Qur'ani jeshini amesema mashindano hayo yako katika vitengo vya qiraa, hifdhi, tafsiri, ufahamu wa Qur'ani na Adhana. Amesema mashindano hayo yatawashirikisha maafisa wa jeshi la nchi kavu, anga na majini baada ya mashindano ya mchujo.
Washiriki watashindana katika vitengo vya tarteel, hifdhi ya juzuu 3, 4, 5, 10, 20 na 25 pamoja na kuhifadhi Qur'ani kamili. Aidha kutakuwa na mashindano ya adhana.
Ameongeza kuwa washindi wa vitengo mbalimbali watatangazwa na kutunukiwa zawadi Jumatano Disemba 21.
918508