IQNA

Filamu ya Akili Mnemba (AI) Yaeleza Maisha ya Qari Abdul Basit

14:48 - December 20, 2025
Habari ID: 3481686
IQNA – Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu nchini Misri limezindua filamu fupi inayoelezea maisha ya marehemu qari Abdul Basit Abdulsamad, kwa kutumia teknolojia ya akili bandia kuonesha hatua muhimu tangu kuzaliwa kwake hadi kufariki.

Uzalishaji huu umejumuisha siku kadhaa za kazi ya kina ili kuhakikisha viwango vya juu vya usahihi, ubora na umaanwi.

Gazeti la Al-Youm Al-Sabea linaripoti: “Mradi huu ni mafanikio ya kipekee katika kuandika urithi wa Kiislamu na kuenzi shakhsia adhimu wa usomaji wa Qur’an Tukufu kwa kutumia teknolojia za kisasa za akili mnemba.”

Mradi huu umefanyika kwa msaada wa Waziri wa Awqaf wa Misri, Osama Al-Azhari.

Mohamed Al-Bayoumi, Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu, alisimamia maudhui ili kuhakikisha usahihi wa kihistoria na wa kidini.

Filamu hii imepata umaarufu mkubwa katika ulimwengu wa Kiislamu tangu ilipozinduliwa kupitia majukwaa rasmi ya kidijitali ya baraza hilo.

3495774

captcha