IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Jeshi la Iran linahudumia Qur'ani Tukufu

21:18 - January 19, 2023
Habari ID: 3476432
TEHRAN (IQNA) - Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni jeshi linaloitekeleza mafundisho ya Qur'ani Tukufu sambamba na kuitumikia.

Hayo yamedokezwa  Alhamisi  mjini Tehran na Hujjatul Islam Abbas Mohammadhassani Mkuu wa Kitengo cha Kiitikadi na Kisiasa katika Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika hafla kwa ajili ya kuhitimisha mashindano ya 42 ya Qur'ani Tukufu ya wafanyakazi wa jeshi.

Ameongeza kuwa Jeshi la Iran daima ni la ushindi na halishindwi kwa sababu ni Jeshi la Qur'ani na limeunganishwa na Kitabu hicho Kitukufu.

Hujjatul Islam Abbas Mohammadhassani  amepongeza anga ya Qur'ani katika Jeshi la Iran na kuwapongeza askari wote wanaohusika na shughuli za Qur'ani na wale walioshiriki katika mashindano hayo.

Alisema mashindano ya Qur'ani ni mashindano pekee ambayo hakuna mshindwa kwa sababu wote wanaoingia katika mashindano hayo ni washindi.

Aidha ameongeza kuwa, yeyote mwenye kuifahamu Qur’ani Tukufu, maisha yake binafsi na ya kijamii yatajawa na nuru.

Kwa mujibu wa Kanali Mehdi Meydani, Mkuu wa Idara ya Qur'ani, Etrat na Sala katika Kitengo cha Kiitikadi na Kisiasa jeshini, mashindano ya mwaka huu yalifanyika katika hatua tatu, huku washiriki 367 wakifuzu katika duru ya mwisho.

Alisema walishindana katika kategoria kadhaa, ikiwa ni pamoja na usomaji wa Qur'ani, Tarteel, kuhifadhi (katika viwango tofauti), na Tafsir (Tafsiri ya Qur'ani).

Washindi wa kategoria tofauti walitunukiwa zawadi za fedha taslimu na vyeti vya heshima katika hafla ya kufunga mashindano.

4115767

 

captcha