Kwa mujibu wa tovuti ya ladepeche, viongozi wa Kanisa la mji wa Albi wameshirikiana na Jumuiya ya Wapenzi wa Uislamu ya mji huo katika hatua hiyo nzuri ya kuchapisha kwa mwaka wa nne mfululizo kalenda hiyo ya Kiislamu na Kikristo ya mwaka huu wa 2012 Milaadia na 1233 Hijiria.
Wahusika wanasema kuwa wamechapisha kalenda hiyo kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na umoja kati ya wafuasi wa dini mbili hizi muhimu za mbinguni. Wanasema minasaba na sikukuu zote muhimu za dini mbili hizo zimeainishwa kwenye kalenda hiyo.
Kalenda hiyo pia inaonyesha maeneo matakatifi ya Kiislamu na Kikristo, jambo ambalo linawawezesha Waislamu wa Ufaransa kufahamu utamaduni na mila za wafauasi wa dini hizi tukufu. 927216