IQNA

Jimbo la Cuebec lalaani mashambulizi yanayofanywa dhidi ya maeneo ya ibada ya Waislamu

17:07 - January 08, 2012
Habari ID: 2253388
Serikali ya jimbo la Cuebec nchini Canada imetoa taarifa likilaani mashambulizi yaliyofanywa na watu wasiojulikana dhidi ya msikiti wa mji wa Gatino.
Waziri wa Uhamiaji wa Cuebec Kathleen Weil amesema kuwa serikali ya jimbo hilo inalaani vikali mashambulizi yanayofanywa dhidi ya misikiti na vituo vya kidini na inatangaza kuwa vitendo kama hivyo haviwezi kuvumiliwa.
Ameongeza kuwa harakati za kibaguzi, kueneza utumiaji mabavu, chuki na mashambulizi dhidi ya vituo vya Kiislamu havioani na mfumo unaotawala Cuebec uliojengeka juu ya misingi uadilifu na mazungumzo kati ya raia na dini mbalimbali.
Wakati huo huo Baraza la Canada na Uhusiano wa Kiislamu na Marekani (CAIR-CAN) limetoa taarifa likitangaza kuwa Msikiti wa Gatino umeshambuliwa mara mbili katika kipindi cha siku tatu na nara zinazokebehi Waislamu zimeandikwa katika kuta za eneo hilo la ibada. Taarifa hiyo imesema, mara ya pili washambuliaji hao wamejaribu kuchoma moto msikiti huo na magari ya Waislamu.
Taarifa hiyo ya CAIR-CAN imesisitiza kuwa hii si mara ya kwanza kwa makundi yenye misimamo mikali kushambulia vituo vya kidini vya Waislamu; baraza la CAIR-CAN linalaani vikali mashambulizi haya na linaitaka serikali ya Canada kutafuta suluhisho la kivitendo la kukabiliana na wimbi la hujuma dhidi ya Uislamu. 930962
captcha