IQNA

Sheikh Naeem Qasim:

Umoja wa Mataifa ni chombo cha Marekani

18:49 - January 11, 2012
Habari ID: 2255733
Naibu Katibu Mkuu wa chama cha Hizbullah cha Lebanon Sheikh Naeem Qasim amesema kuwa Umoja wa Mataifa na Katibu Mkuu wake ni watekelezaji wa siasa na matakwa ya Wamarekani na hawawakilishi jamii ya kimataifa.
Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ameyasema hayo leo katika semina ya 'Vita Laini' iliyofanyika mjini Beirut na kusema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anawakilisha maslahi ya Marekani na si mwakilishi wa nchi zote duniani.
Akijibu swali kwamba je, safari ya Ban Ki-moon nchini Lebanon ni sehemu ya vita laini, Sheikh Qasim amesema iwapo tutaiita kuwa ni vita laini basi tutakuwa tumeipa heshima kupita kiasi, lakini ukweli ni kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anakuja Lebanon kukamilisha mipango ya Marekani na kutekeleza siasa zake. 933747



captcha