IQNA

Ayatullah Kashani:

Maadui wanahofia mno nafasi ya kielimu ya Iran

1:30 - January 14, 2012
Habari ID: 2256421
Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amelaani vikali mauaji ya mwanasayansi wa nyuklia wa Kiirani aliyeuawa na vibaraka wa ubeberu na Uzayuni wa kimataifa.
Ayatullah Muhammad Imami Kashani amesema hayo mbele ya hadhara ya waumini waliohudhuria ibada ya Sala ya Ijumaa mjini Tehran na kusisitiza kwamba, nafasi ya kielimu ya Iran imewatia woga na wahaka mkubwa maadui.
Ayatullah Kashani ameashiria uhasama na chuki ya maadui dhidi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusema, maadui hawataki kuona Iran ina mamlaka ya kujitawala na yenye maendeleo na ndio maana hivi sasa wameanzisha njama maalumu ya kuwauwa wasomi na wanasayansi wa Kiirani.
Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran ametoa mkono wa pole kwa tabaka la wasomi nchini Iran kwa mnasaba wa kuuawa shahidi Mustafa Ahmadi Roshan mwanasayansi wa nyuklia wa Kiirani na kutaka kushtakiwa katika vyombo vya kimataifa waliohusika na jinai hiyo.
Katika upande mwingine, Ayatullah Imami Kashani ametaka wananchi wa Iran kuwa macho na njama za maadui dhidi ya Mapinduzi ya Kiislamu na kubainisha kwamba, umoja na mshikamano unapaswa kusambaratisha njama chafu za maadui dhidi ya taifa hili. 934417
captcha