IQNA

Ikhwani Misri waitahadharisha Marekani

14:18 - January 15, 2012
Habari ID: 2256852
Kiongozi mmoja wa chama cha Uhuru na Uadilifu tawi la harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Misri ameitaka Marekani itazame upya uungaji mkono wake kwa utawala ghasibu wa Israel na kusisitiza kuwa kuendelea kuuungaji mkono utawala huo haramu kunahatarisha maslahi ya Washington katika Mashariki ya Kati.
Jamal Tajuddin amesema kuwa Marekani inapaswa kutambua kwamba, nchi za Kiarabu ambazo zimekumbwa na mapinduzi ya wananchi hazitakuwa tena tegemezi kwa serikali ya Washington.
Ameongeza kuwa Marekani inapaswa kuelewa kwamba sasa wananchi Waarabu ndio wanaochukua uamuzi kuhusu masuala ya nchi zao na si tawala za nchi hizo, kwa msingi huo uhusiano wa Misiri na Marekani unapaswa kuwa sawa na kuheshimu maslahi ya pande mbili, na si kujali maslahi ya Marekani na Israel pekee.
Kuhusu ziara ya Naibu Waziri wa Marekani William Burns katika ofisi za chama cha Uhuru na Uadilifu mjini Cairo, Tajuddin amesema lengo la ziara hiyo lilikuwa kutaka kujua mitazamo ya chama hicho kuhusu masuala ya ndani na ya kieneo.
Ameongeza kuwa Marekani inataka kutambua vyema vyama vipya vya Misri kwa sababu inajua kwamba vyama hivyo vitakuwa na nafasi muhimu katika medani za kisiasa na kuwa na taathira katika misimamo ya kisiasa ya Misri nje ya nchi. 934346
captcha