Kwa mujibu wa tovuti ya CPI Ekmeleddin Ihsanoglu, Katibu Mkuu wa OIC amelaani vikali shambulio hilo lililofanywa na Wazayuni katika msikiti wa kijiji cha Dirastia pamoja na maandishi ya chuki dhidi ya Uislamu na ubaguzi wa rangi waliyoandika kwenye kuta za msikiti huo.
Amesema katika sehemu ya taarifa hiyo kwamba utawala ghasibu wa Israel unapasa kubeba lawama za hujuma hiyo na kuwajibika mbele ya hujuma za mara kwa mara zinazofanywa na walowezi wa Kizayuni dhidi ya maeneo ya ibada na Wapalestina wasio na hatia.
Katibu Mkuu wa OIC ameendelea kusema kuwa hujuma hiyo ni matokeo ya ugaidi uliopangwa dhidi ya Wapalesina na matukufu ya Kiislamu, hujuma ambayo amesema haiwezi kutekelezwa bila ya uungaji mkono wa utawala wa Tel Aviv.
Wakati huohuo OIC pia imelaani kuingia hivi karibuni askari wa utawala huo katika Msikiti wa al-Aqsa na kusema hatua hiyo ni sawa na kuvamiwa vituo vya Kiislamu. Imeongeza kuwa Msikiti wa al- Aqsa ni mstari mwekundu kwa Waislamu wote na kwamba kuendelea kwa uchokozi wa Wazayuni katika maeneo matakatifu ya Waislamu hakutakuwa na matokea mazuri. 934831