IQNA

Mwamko wa Kiislamu wakamilisha mwaka mmoja

14:49 - January 16, 2012
Habari ID: 2257910
Wananchi wa Tunisia wameadhimisha mwaka mmoja tangu kufanyika mapinduzi ya wananchi nchini humo.
Mwandishi wetu ameripoti kuwa, maelfu ya wananchi wa Tunisia Jumamosi iliyopita walimiminika mabarabarani nchi nzima na kusherehekea mwaka mmoja wa ushindi wa mapinduzi ya wananchi yaliyoung'oa madarakani utawala wa muda mrefu wa dikteta Zainul Abidin Bin Ali aliyekimbilia Saudi Arabia. Watunisia wengi walivaa nguo nyekundu na nyeupe, rangi ambazo ziko kwenye bendera ya nchi yao na kutoa nara mbalimbali.
Vuguvugu la mapinduzi ya Tunisia lilianzia katika mji wa Sidi Bouzid ambako kijana mmoja msomi alijichoma moto katika kulalamikia dhulma na ukatili wa maafisa usalama wa utawala wa nchi hiyo. Tukio hilo liliibua harakati ya wananchi wa Tunisia dhidi ya utawala wa kifisadi wa Zainul Bin Ali na hatimaye tarehe 14 Januari mwaka uliopita wa 2011 dikteta huyo alikimbilia Saudi Arabia.
Kwa manasaba wa siku hiyo Rais mpya wa Tunisia Munsif al Marzouqi amesisitiza kwamba, serikali ya nchi hiyo itaendelea kufuata njia ya demokrasia na kufanikisha malengo ya mapinduzi ya wananchi. 935318



captcha