Kiongozi wa kundi lenye misimamo ya kufurutu mipaka la Shas, Kuhani Ovadia Yosef amesema anaomba dua ya kuachiwa huru Hosni Mubarak, wakati taifa la Misri likiandamana na kuvitaka vyombo vya mahakama vya nchi hiyo vimhukumu kifo dikteta huyo.
Kuhani Ovadia Yosef amedai kuwa Mubarak ameipa fahari na heshima serikali ya Misri na sasa amepinduliwa, na Wayahudi wanapaswa kuomba dua ya kuachiwa kwake huru na kumuomba Mwenyezi Mungu awape majaji wa Misri hekima na maarifa ili wasimamishe kesi yake na kufuta mashata yanayomkabili.
Kuhani Yosef amesema: "Zaidi ya miaka 28 iliyopita nilikutana na kuzungumza na Hosni Mubarak na baada ya mazungumzo hayo na kukubaliana katika masuala yote nilibakia mimi na Mubarak ofisini kwake katika ikulu ya Rais mjini Cairo kisha akaniambia: Niombee dua, hakika mimi nina imani na dua yako."
Kuhani huyo anaendelea kusimulia kwamba: "Niliweka mkono wangu juu ya kichwa cha Hosni Mubarak kisha nikamuombea dua. Tukio hili lilijiri miaka 28 iliyopita, na kubakia kiongozi madarakani miaka 30 nchini Misri si jambo la kawaida, kwa msingi huo hapana shaka kuwa jambo hilo limetokana na dua niliyomuombea"!
Ushindi wa vyama vya Kiislamu katika chaguzi za Misri umewatia kiwewe viongozi wa nchi za Magharibi na utawala wa Kizayuni wa Israel ambao ameuhudumia kwa miaka mingi.
935768