Ahmadinejad amesisitiza kwamba, kustawishwa uhusiano na nchi za Amerika ya Latini kunafanyika kwa lengo la kukuza ushirikiano na nchi zinazojitawala katika uga wa kimataifa ili kukabiliana na hatua za kupenda makuu za mfumo wa kibeberu.
Rais Ahmadinejad amesema hayo katika kikao cha baraza lake la mawaziri na kusisitiza juu ya udharura wa kufuatiliwa kwa makini utekelezwaji wa hati za makubaliano zilizotiwa saini baina ya Iran na nchi za Latini Amerika katika safari yake ya hivi karibuni katika nchi hizo.
Dakta Ahmadinejad amesema katika kikao na baraza lake la mawaziri kwamba, safari yake huko Latini Amerika ilikuwa na mafanikio makubwa mno.
Alkhamisi iliyopita Rais Ahmadinejad alikamilisha safari yake ya kuzitembelea nchi nne za eneo la Amerika ya Latini yaani Venezuela, Cuba, Nicaragua na Ecuador.
936010