IQNA

Warsha ya 'Kituo cha Kiislamu cha al Azhar na Afrika, Changamoto na Mustakbali' kufanyika Cairo

17:26 - January 18, 2012
Habari ID: 2259488
Warsha ya Kituo cha Kiislamu cha al Azhar na Afrika, Changamoto na Mustakbali itafanyika tarehe 30 Januari kwa ushirikiano wa Chuo cha al Azhar na Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri.
Warsha hiyo itasimamiwa na Mkuu wa al Azhar Ahmad Tayyib na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Muhammad Kamil Amru.
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Masuala ya Idara ya Jumuiya ya Kimataifa ya Wanafunzi wa Chuo cha al Azhar Usama Yasin amesema kuwa warsha hiyo itajadili mchango wa kijamii, elimu na utamaduni wa Kituo cha Kiislamu cha al Azhar, changamoto zinazokabili siasa za Misri barani Afrika na mikakati ya kuanzisha siasa mpya.
Usama Yasin amesema wasomi na wataalamu wa Kimisri watashiriki katika warsha hiyo. 937653

captcha