Ripoti zinasema kuwa watu wanaopiga vita Uislamu walishambulia eneo hilo lililoko kaskazini mwa Ufaransa na mbali na kuandika maneno machafu katika kuta zake, walichora pia msalaba uliovunjia na alama ya Manazi wa Ujerumani katika kuta za msikiti na Kituo hicho cha Kiislamu.
Polisi ya Ufaransa imesema kuwa imeanza uchunguzi wa kadhia hiyo lakini bado haijapata ishara yoyote kuhusu watu waliohusika na uhalifu huo.
Ujenzi wa msikiti na Kituo cha Kiislamu cha mji wa Montigny-en-Ostrevent ulianza mwaka 2010 na kitafunguliwa miezi mitatu ijayo. 937412