IQNA

Walibya waandamana wakitaka sheria za Kiislamu zitumike nchini humo

8:35 - January 22, 2012
Habari ID: 2260859
Mamia ya watu wa Libya wameitisha maandamano wakiwataka viongozi wa nchi hiyo kutekeleza sheria za Kiislamu.
Maandamano yamefanyika katika mji mkuu Tripoli na miji ya mashariki mwa nchi hiyo ya Benghazi na Sabha.
Huku wakiwa wameinua Qur’ani Tukufu, waandamamaji wametoa nara za kuitaka serikali ya mpito nchini humo kutegemea sheria za Kiislamu wakati wa kuandika katiba mpya. Aidha wametaka kuwepo kipengee katika katiba kinachotambua Uislamu kama dini rasmi ya serikali. Wanaharakati wa Kiislamu Libya wanasema wameamua kuandamana baada ya kubainika kuwa vyama vya Kisekula vinavyoungwa mkono na Wamagharibi vimeundwa nchini humo. Itakumbukwa kuwa Waziri Mkuu wa Muda wa Libya Abdel Rahim al-Kib alipoingia madarakani mwezi Novemba mwaka jana alisema serikali mpya ya Libya itazingatia sheria za Kiislamu.
Habari zaidi kutoka Libya zinasema Marekani imetuma wanajeshi 12,000 nchini Libya katika awamu ya kwanza ya kutuma vikosi vyake katika nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika yenye utajiri wa mafuta.
Ndiyo kusema kwamba ushindi wa wanaharakati wa Kiislamu katika chaguzi za Misri, Tunisia na Morocco umedhihirisha wazi kuwa wimbi la mwamko wa Kiislamu katika Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika ni ukweli usioweza kukanushika.../
938553
captcha