Mtandao wa Afreeknews umeripoti kuwa karibu watu elfu tatu wameshiriki katika maandamano hayo ikiwa ni kwa mara kadhaa sasa wakitaka kutumiwa sheria za Kiislamu katika kubuni katiba mpya ya Libya.
Waandamanaji hao walibeba nakala za Qur’ani na kupiga nara zinazotoa wito wa kutekelezwa sheria za Kiislamu nchini Libya.
Vilevile walitawanya ujumbe uliosisitiza juu ya udharura wa kutekelezwa sheria za Kiislamu nchini humo na kuwataka viongozi wa Libya kutilia maanani suala hilo. Waandamanaji hao wamesisitiza kuwa suala la utekelezaji wa sheria za Kiislamu halihitaji hata kupigiwa kura ya maoni.
Awali Kiongozi wa Baraza la Mpito la Libya Mustafa Abduljalil alitangaaza kuwa sheria za Kiislamu zitakuwa chanzo kikuu cha sheria za Libya baada ya kun’golewa madarakani utawala wa kidikteta wa Muammar Gaddafi. 938553