Kwa mujibu wa tovuti ya Al Manar, televisheni za satalaiti za Kiarabu zitashiriki katika maandamano hayo kwa kurusha hewani vipindi vya kuunga mkono Quds Tukufu.
Jumuiya ya Watayarishaji Vipindi wa Vyombo vya Habari vya Kiarabu imetoa taarifa na kusema maandamano hayo yanafanyika kwa lengo la kubainisha mshikamano na Quds Tukufu.
Mkuu wa Jumuiya hiyo Ebrahim Abu Zhikri amesema hii ni hatua kubwa katika kuunga mkono Qibla cha kwanza cha Waislamu. Ameongeza kuwa wanakusudia pia kutetea Quds kama mji mkuu wa kudumu wa taifa la Palestina.
Ameendelea kusema kuwa Ijumaa Machi Pili televisheni zote za satalaiti za Kiarabu zitaacha kutangaza matangazo yao ya kawaida na mahala pake kutakuwa na matangazo ya moja kwa moja ya kuonyesha mshikamano na watu wa Quds pamoja na miji na maeneo mengine ya Palestina.
940634