Mkutano huo utafanyika kwa hima ya Kituo cha Kiislamu cha mji wa Strasbourg ukihudhuriwa na maulamaa, wasomi na wanafikra na Waislamu wa Ufaransa.
Miongoni mwa ratiba za mkutano huo ni pamoja na programu za kasida za kundi la Asala, vikao vilivyopewa jina la "Mtume wa Uislamu, Nembo ya Fikra Huru", tungo za kumsifu Mtume, hotuba za maulamaa mashuhuri wa Kiislamu na maonyesho ya vitabu vinavyohusu sira na maisha ya Mtume.
Sehemu nyingine ya mkutano huo itahusu mashindano ya watoto na vijana itakayokuwa na maudhui ya 'Mtume Muhammad (saw) katika Mtazamo wa Watoto'. 941608